Michuano ya Kombe la Dunia bado inaendelea huko nchini Urusi huku ikiwa imefikia hatua ya nusu fainali mpaka sasa na tayari nyota saba kutoka Chelsea wanaoziwakirisha timu zao za taifa kwenye michuano hiyo wamefanikiwa kuzisaidia timu zao kufika hatua ya nusu fainali ambapo michezo yake itaendelea tarehe 10-Julai na tarehe 11-Julai.
Lakini mpaka kufikia sasa tovuti ya takwimu michezo maarufu kama Whoscored.com imetoa takwimu kwa nyota waliofanya vizuri kwenye michuano hiyo ambayo kiuhakika inamuonyesha winga wa timu ya Chelsea anayeiwakilisha timu ya taifa ya Ubelgiji kwenye michuano hiyo akiwa pia ndiye nahodha mkuu wa timu hiyo, Eden Hazard ndiye anaongoza kwenye orodha ya wachezaji waliofanya vizuri.
Mtandao au tovuti hiyo imempa Hazard wastani wa 8.56 wa kufanya vizuri, Yeri Mina ambaye ni mlinzi wa Colombia anafuata akiwa na wastani 8.35 wakati nyota wa tatu ni Isco Alcorn ambaye ameiongoza timu ya Hispania ambaye yeye amepewa wastani wa 8.29
Hii inamaanisha nini? kawaida ya takwimu huwa hazikosani sana kwa maana hiyo huenda chama cha soka duniani (FIFA) kikamchagua Hazard kuwa mchezaji bora wa Kombe la Dunia mwaka huu na usisahau wapinzani wake Yeri Mina na Isco wote washatupwa nje kwenye michuano hiyo.
Ameiongoza Ubelgiji kwenye michezo minne huku akifunga magoli mawili na kutengeneza mengine mawili kwa kutoa pasi za mwisho lakini pia ndiye mchezaji aliyevunja rekodi ya kukokota mpira (dribbling) zaidi katika mchezo mmoja, akikokota mara 10 huku akikokota kwa uhakika wa 100%
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment