Chelsea yatua kwa nyota wa Croatia - Darajani 1905

Chelsea yatua kwa nyota wa Croatia

Share This

Klabu ya Chelsea inatajwa kuingia kwenye mashinda au vita ya kumuwania nyota mlinzi wa kikosi cha timu ya taifa ya Croatia ambacho kimefanikiwa kufudhu kucheza nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka huu, Filip Benkovic.

Chelsea inatajwa kuingia kwenye vita hiyo ya kumfukuzia mlinda mlango huyo mwenye miaka 23 anayetajwa pia kuwepo kwenye mipango ya klabu ya AC Milan inayopewa nguvu na wakala wa nyota huyo raia wa Italia, Bepe Bozzo ambaye anatajwa kutumika kwenye ushawishi wa kusajiliwa kwa nyota huyo.

Benkovic ambaye jina lake la utani ni 'Big Ben' kutokana na ukubwa wa mwili wake anaichezea klabu ya Dinamo Zagreb na kuna taarifa kuwa klabu hiyo inahitaji kiasi cha euro milioni 23 mpaka 30 ili iweze kumuuza nyota wao huyo.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu za
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment