Huenda wengi wamechanganywa juu ya habari zilizosambaa jana wakati nyota wa Chelsea ambao hawakuungana na timu zao za taifa kurejea klabuni Chelsea na kuanza mazoezi mepesi kabla ya kuanza michezo ya kirafiki ambapo kwa upande wa Chelsea watacheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Perth Glory huko nchini Australia.
Kilichowachanganya wengi ni juu ya nyota wa Chelsea kufanya mazoezi bila kuonekana kocha Antonio Conte na wakati wengi wakiamini anajiandaa kuondoka ikatolewa taarifa ambayo hata huku niliileta kutoka kwa mwandishi wa habari za michezo anayeaminika Matt Law akisema kocha huyo alifika klabuni Chelsea ingawa hakuungana na wachezaji.
Nilipoituma habari hiyo nikapata mfululizo wa maswali wengi wakinifata kuniuliza kuhusu habari hii.
Hatimaye leo tena tovuti ya habari za michezo za Chelsea, Breathe Chelsea imetoa ripoti kwamba kocha huyo hakuonekana jana kutokana na maagizo aliyopewa kwamba ataanza kusimamia mazoezi siku ya jumatatu.
Sasa katika hili bado haijaeleweka kama yeye ndiye kaomba aanze mazoezi jumatatu au uongozi wa bodi ambao unadaiwa kumfukuzia kocha Maurizzio Sarri ili achukue mikoba ya Conte ndio umeagiza kocha huyo aanze kufanya kazi siku ya jumatatu, hapo jibu bado sijalipata.
Lakini pia ukichunguza kauli aliyokaririwa kocha huyo aliposema anawaagiza wachezaji warejee klabuni jumatatu na sio jumamosi au jumapili huenda yeye kocha ndio alipanga kuanza kazi jumatatu na sio jumamosi au jumapili kama ilivyoagizwa na moja ya viongozi wa bodi.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment