Mchezo wa soka umekuwa ukivuta hisia za watu wengi haswa kutokana na burudani inayopatikana kwenye michuano hiyo. Moja kati ya burudani inayonogesha mchezo huo ni utabiri unaofanywa na wanyama katika mchezo huo wa soka.
Aina hii ya burudani haina muda mrefu kwenye michezo haswa mchezo wa soka na basi kama ni maarufu haukuwai kuteka hisia za watu wengi kama ilivyo miaka hii ya karibuni.
Naamini wote tunamkumbuka sana yule pweza aliyebatizwa jina la Pol ambaye alitumika kwenye utabiri kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 huko nchini Afrika Kusini akihusika kwenye utabiri wa michezo mingi kabla ya baadae kupoteza maisha. Lakini baadae tena tukamsikia ng'ombe akitumika kutabiri lakini akaja kubugi alipotabiri fainali ya ligi ya Ulaya (Europa League) alipotabiri Ajax ya Uholanzi itaifunga Man utd lakini utabiri wake ukaenda vibaya. Hiyo ilikuwa msimu wa 2016-2017.
Sasa mwaka huu alijitokeza mwengine ambaye alikuwa paka aliyefanya utabiri lakini mwisho wa siku naye akabugi.
Lakini kuna hii inamhusu nyota wa Chelsea, Eden Hazard ambaye hapa nampa jina la pweza 'Paul the Octopus' mara baada ya utabiri wake alioufanya wa Kombe la Dunia mwaka huu kukaribia kwenda sahihi kwa 90%
Tukiachana na huko kwenye hatua ya robo fainali na 16 bora ambapo kidogo alitabiri tofauti na ilivyotokea lakini kwenye hatua ya nusu fainali na fainali imebaki kidogo tu ikamilike.
Alitabiri Ubelgiji itakuwa mabingwa lakini kwenye hatua ya fainali itacheza dhidi ya Uingereza, utabiri ambao kuna uwezo kukamilika maana timu hizo zinacheza nusu fainali huku Ubelgiji ikicheza dhidi ya Ufaransa mchezo ambao pia alitabiri utatokea kwenye hatua ya nusu fainali wakati Uingereza ikicheza dhidi ya Croatia ila hapa alitabiri Uingereza itacheza dhidi ya Argentina.
Je Hazard anafaa kutumika kututabiria bingwa wa ligi kuu msimu ujao? 😁😁😁😁Hazard kawa pweza
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment