Kombe la Dunia; Uingereza yakamilisha nyota 7 wa Chelsea kwenye nusu fainali - Darajani 1905

Kombe la Dunia; Uingereza yakamilisha nyota 7 wa Chelsea kwenye nusu fainali

Share This

Jana kulichezeka michezo miwili ya kukamilisha hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2018 inayoendelea huko nchini Urusi.

Mchezo wa kwanza ulikuwa mchezo uliowahusisha nyota wawili wa Chelsea ambao ni Gary Cahill na Ruben Loftus-Cheek ingawa hawakupata nafasi ya kuichezea timu yao ya Uingereza ilipomenyana dhidi ya Sweden na kuishuhudia Uingereza ikipata ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Harry Maguire anayeichezea klabu ya Leicester city pamoja na Delle Alli wa Tottenham.

Ushindi huo unaamisha timu hiyo imefudhu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo itamenyana dhidi ya Croatia walioshinda kwa penati dhidi ya wenyeji Urusi.

Ratiba ya Nusu fainali;
Ufaransa vs Ubelgiji
Tarehe 10-Julai
Ufaransa; N'Golo Kante na Olivier Giroud
Ubelgiji; Eden Hazard, Michy Batshuayi na Thibaut Courtois

Uingereza vs Croatia
Tarehe 11-Julai
Uingereza; Gary Cahill na Ruben Loftus-Cheek

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment