Uchambuzi: Kuelekea West Ham vs Chelsea (23-Septemba-2018) - Darajani 1905

Uchambuzi: Kuelekea West Ham vs Chelsea (23-Septemba-2018)

Share This

Tumekuwa na mfululizo wa kuchambua michezo ya ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2018-2019 ambayo Chelsea itakuwa ikicheza.

Toka tumeanza mpaka kufikia leo tunaenda kuchambua mchezo wa sita, mchezo utakaozikutanisha klabu mbili kutoka jiji moja, jiji la London ambapo Chelsea itasafiri mpaka kwenye uwanja wa London Stadium na kushuhudia ikicheza dhidi ya West Ham united itakayokuwa nyumbani siku hiyo.

Msimu uliopita West Ham waliisumbua Chelsea ambapo kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa London Stadium uliisha kwa Chelsea kupoteza kwa goli 1-0 lililofungwa na Arnautovic wakati kwenye mchezo wa pili ambao ulichezwa Stamford Bridge, Chelsea ikafanya uzembe kumruhusu Javier Hernandez 'Chicharito' kufunga goli la kusawazisha na kufanya mchezo kwenda sare ya 1-1.

Mchezo huu utachezwa kwa kukamiana sana haswa kutokana na utani wa kutokea jiji moja.

Kihistoria inasema katika michezo mitano ya mwisho, Chelsea imeshinda michezo miwili huku ikipoteza michezo miwili huku mchezo mwengine wakitoka sare. Lakini kijumla klabu hizo zimekutana mara 110 huku Chelsea ikishinda michezo 49 na kupoteza 40 wakati ikitoa sare michezo 21.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment