"Mimi bado ni kocha wa Chelsea, nataka wachezaji waanze kurejea kuanzia jumatatu" ni kauli inayodhaniwa kutolewa na kocha wa Chelsea, Antonio Conte akipinga taarifa iliyotolewa na moja ya viongozi wa bodi ya Chelsea ambaye aliwatumia ujumbe nyota wote wa Chelsea ambao hawajashiriki michuano ya Kombe la Dunia akiwaambia warejee klabuni siku ya jumamosi na jumapili.
Lakini jambo la kushangaza kocha huyo anaripotiwa kufika klabuni Chelsea hii leo akiendelea kuwa kocha wa Chelsea, klabu ambayo anamalizana nayo mwishoni mwa msimu huu kutokana na mkataba wake kubakisha mwaka mmoja.
Amefika kwenye viwanja vya mazoezi vya Chelsea maarufu kama Cobham Stadium akiwa pamoja na nyota wa Chelsea waliotimiza wajibu wa kuripoti klabuni siku ya leo (jumamosi) na kesho tarehe 8-Julai.
Kauli zinapishana katika swala hili, inawezekana kinachoendelea kwa sasa ni kama magazeti na vyombo vya habari kuchochea kuondoka kwa kocha huyo.
Na hilo aliwai kuliongelea alipohojiwa mara baada ya mchezo wa Chelsea dhidi ya Barcelona kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa Ulaya ambapo aliwalalamikia waandishi wa habari waliokosoa aina ya soka ambalo Chelsea ilicheza kwenye mchezo huo ulioisha kwa sare ya 1-1 ambapo walisema Chelsea imecheza soka la kuzuia sana hivyo kucheza soka bovu.
Hilo alilijibu kwa hasira kwa kuwaita waandishi hao hawajui soka na ndio maana walimsema vibaya kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger kwa kuruhusu kufungwa mfululizo magoli 3-0 na klabu ya Manchester city wakati yeye amefanikiwa kutoka nao sare hiyo ya 1-1 na bado wanamsema vibaya, kwa hiyo walitaka nae afungwe kama Wenger?
Mwandishi Matt Law ametuma ujumbe akitaarifu kwamba kocha huyo haonekani kuwa na dalili ya kuondoka Chelsea na huenda hilo swala la nafasi yake kuchukuliwa na Maurizzio Sarri likabaki kuwa tetesi. Mwandishi huyo ameripoti pia kwamba kocha huyo amefika Chelsea ingawa bado hajaanza mazoezi rasmi na nyota waliofika.
Nyota wa Chelsea waliofika klabuni Chelsea na kuanza mazoezi ni pamoja na Cesc Fabregas, David Luiz, Tiemoue Bakayoko, Emerson Palmieri, Marcos Alonso, Davide Zappacosta, Alvaro Morata, Pedro Rodriguez, Callum Hudson-Odoi, Ethan Ampadu, Kasey Palmer, Fokoyi Tomori, Ola Aina, Charly Musonda Jr na wengine wengi.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment