Kombe la Dunia; Gary Cahill, Loftus-Cheek kutimiza nyota saba nusu fainali? - Darajani 1905

Kombe la Dunia; Gary Cahill, Loftus-Cheek kutimiza nyota saba nusu fainali?

Share This

Jana ilikuwa siku tamu kwa nyota wa kikosi cha timu ya Ubelgiji mara baada ya kufudhu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu inayoendelea huko nchini Urusi kwa kuibamiza timu ya taifa ya Brazil.

Kupata ushindi huo wa mabao 2-1 kulimaanisha nyota watatu wa Chelsea wanaoichezea timu hiyo ya Ubelgiji wamefanikiwa kufudhu kucheza nusu fainali. Ukijumlisha na nyota wengine wawili wa Ufaransa, N'Golo Kante na Olivier Giroud nao waliofanikiwa kufudhu kucheza hatua hiyo ya nusu fainali ambapo jumla inawafanya nyota watano wa Chelsea wametangulia kucheza nusu fainali mwaka huu.

Sasa jioni ya leo muda wa saa 17:00 kunachezwa mchezo mwengine wa robo fainali kati ya Sweden wanaocheza dhidi ya Uingereza.

Nyota wengine wawili wa Chelsea watakaoiongoza timu ya Uingereza kucheza kwenye mchezo huo ni Gary Cahill na Ruben Loftus-Cheek na kama wakifanikiwa kufudhu hatua hiyo basi iyo itamaanisha nyota saba wa Chelsea wamefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment