Courtois atoa neno kuhusu kauli yake kwa nyota wa Uingereza - Darajani 1905

Courtois atoa neno kuhusu kauli yake kwa nyota wa Uingereza

Share This

Tarehe 28-Juni mwaka huu kulichezwa mchezo wa mwisho wa kundi G katika michuano ya Kombe la Dunia ikizikutanisha timu ya Ubelgiji dhidi ya Uingereza ambapo mchezo huo uliisha kwa Ubelgiji ikishinda 1-0, goli lililofungwa na winga Adnan Januzaj. Nadhani wengi tunakumbuka haswa wengi wakikerwa na vikosi vilivyopangwa na timu zote ambavyo haviwahusisha nyota waliotegemewa kutokana na timu zote kujihakikishia kufudhu hatua hiyo ya makundi.

Mara baada ya mchezo huo, mlinda mlango wa klabu ya Chelsea ambaye ni mlinda mlango nambari moja wa Ubelgiji, Thibaut Courtois ambaye kwa siku hiyo alikuwa nahodha wa Ubelgiji alifanyiwa mahojiano na katika mahojiano hayo alisema goli walilofungwa Uingereza kama angekuwa yeye ndiye mlinda mlango wa timu hiyo basi angeweza kuokoa goli hilo.

Mara baada ya kauli hiyo ziliibuliwa shutma nyingi kuhusu kauli hiyo ambapo ilikuwa inaripotiwa kwamba nyota huyo amemdharau mlinda mlango wa Uingereza, Jordan Pickford kwamba sio mlinda mlango mzuri.

Lakini Courtois ameibuka na kutoa neno kuhusu shutma anazopatiwa.

"Kiukweli nasikitishwa na taarifa zinazosambaa kwamba mimi nimemdharau Pickford, hapana nahitaji kuweka sawa maana nilichokimaanisha ni kama kinatafsiriwa tofauti. Nilisema kwamba mimi ningeweza kuokoa kwa kuwa mimi ni mrefu kuliko Pickford, lakini Pickford ni nyota mzuri na namheshimu" alisema Courtois.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment