Jana usiku kulichezeka mchezo wa hatua ya robo fainali kati ya Ubelgiji dhidi ya Brazil na kushuhudiwa Brazil ikitupwa nje ya michuano hiyo ya Kombe la Dunia mara baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1.
Wote tunafahamu kwamba Ubelgiji ndiyo timu yenye wachezaji wengi kutoka Chelsea kwa Kombe la Dunia mwaka huu ambapo ina nyota watatu ambao ni Eden Hazard, Thibaut Courtois pamoja na Michy Batshuayi.
Sasa huko mtandaoni jana kulikuwa na kituko kilitokea mara baada ya Ubelgiji kupata ushindi huo na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya nusu fainali ya Kombe hilo linalofanyika huko nchini Urusi.
Mara baada ya mchezo kumalizika, kiungo wa Chelsea ambaye mwaka huu hakuchaguliwa kwenye timu yake ya taifa ya Hispania, Cesc Fabregas alitumia ujumbe kupitia mtandao wa Twitter akiwauliza wanaomfatilia (followers), je ni mchezaji gani kutoka Chelsea atabeba Kombe la Dunia mwaka huu huku akiyataja majina yote ya nyota hao ambao ni Eden Hazard, Thibaut Courtois, Michy Batshuayi ambao wote wanaiwakilisha Ubelgiji, Ruben Loftus-Cheek na Gary Cahill ambao wote wanaiwakilisha Uingereza, N'Golo Kante na Olivier Giroud ambao wanaiwakilisha Ufaransa.
Na mmoja wa watu wanaomfatilia alitoa maoni kwa kumuuliza kama aliweza kushuhudia uwezo ulioonyeshwa na Eden Hazard kwenye mchezo dhidi ya Brazil lakini kiungo huyo akamjibu kwa kumwambia hakuweza kuangalia mchezo huo kutokana na safari aliyokuwa nayo ya kurejea klabuni Chelsea akitokea mapumzikoni.
Sasa kituko kilianza pale Michy Batshuayi alipomjibu Fabregas kwa kumwambia inamaana hukuona nilivyofunga magoli matatu? akimuuliza Fabregas lakini Fab naye akajibu kwa kumuuliza hayo magoli umefungia wapi? (Batshuayi hakucheza kabisa mchezo dhidi ya Brazil) ndipo Batshuayi akamjibu kwa kuonyesha kucheka.
Ndipo Fabregas akamaliza mjadala kwa kuwapongeza na kuwapa hongera nyota wenzake kwa kufikia hapo walipo.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment