Juzi nilikuletea taarifa kwamba kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameingia kwenye mtafaruku na bodi ya Chelsea kutokana na kupinga ujumbe uliotolewa na moja ya viongozi wa klabu hiyo ambaye aliwatumia ujumbe (email) nyota wote wa Chelsea ambao hawakushiriki michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko nchini kurejea klabuni mwisho ikiwa siku ya jumapili ili kujiandaa na michezo ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya.
Lakini kocha huyo alipinga na kusema yeye bado kocha wa Chelsea na anawapa muda wachezaji hao ambao hawajashiriki Kombe la Dunia warejee klabuni siku ya jumatatu.
Mtafaruku huu umezidi kuchukua sura mpya mara baada ya baada ya nyota hao kuanza kurejea klabuni.
Cesc Fabregas akitumia mtandao wa Instagram ametuma picha akionyesha kufika jijini London nchini Uingereza akitoka mapumziko ambapo muda mwingi amekuwa sambamba na familia yake.
Lakini pia klabuni Chelsea tayari kuna nyota washarejea na wameshaanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya. Ethan Ampadu, Charly Musonda Jr, Kasey Palmer, Ola Aina, Kenedy, Fokoyi Tomori na nyota wengine wametumia mtandao wa Instagram kutuma picha ikiwaonyesha wakiwa mazoezini kwenye uwanja wa mazoezi wa Cobham Stadium.
Je kauli ya nani itasikilizwa? hilo ambalo tunalisubiri wengi, je kuna mchezaji atarejea klabuni siku ya jumatatu? kama akitokea wa kurejea siku hiyo na asiadhibiwe na klabu basi inamaana kuna nafasi kubwa ya kocha Antonio Conte kusalia kuwa kocha wa Chelsea kwa msimu mwingine akiwa anamalizia mkataba wake.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment