Ushindi wa mabao 1-2 ulioupata timu ya taifa ya Ubelgiji dhidi ya Brazil kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Dunia inamaanisha sasa timu hiyo itapambana dhidi ya Ufaransa ambao wao waliondoka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Uruguay, mchezo wao ukichezwa saa 17:00 kwa saa za Afrika Mashariki wakati huo mchezo wa Brazil dhidi ya Ubelgiji ukichezwa saa 21:00 kwa saa za Afrika Mashariki.
Hii inamaanisha nini kwa nyota wa Chelsea? hii inamaanisha kati ya nyota nane wa Chelsea waliofanikiwa kufudhu kucheza hatua ya robo fainali, ni nyota mmoja ametoka ambaye ni Willian Borges akiwaacha wenzake saba ambao kati ya hao saba wawili wanacheza jumamosi ya leo ya tarehe 7-Julai ambao ni Gary Cahill na Ruben Loftus-Cheek watakaoingoza timu ya taifa ya Uingereza kucheza dhidi ya Sweden.
Nyota watano ambao wameshafuzu nusu fainali ni pamoja na N'Golo Kante na Olivier Giroud wote kutoka Ufaransa, Eden Hazard, Michy Batshuayi na Thibaut Courtois wote kutoka Ubelgiji huku ikiwasubiri wenzao wa Uingereza ili kukamilisha nyota saba.
Rekodi zilizowekwa na nyota wa Chelsea:
➡Tangu mwaka 1966, hakuna mchezaji aliyekokota (dribbling) mara nyingi kwenye mchezo mmoja wa Kombe la Dunia kumzidi Eden Hazard ambaye kwenye mchezo dhidi ya Brazil alikokota mpira mara 10 na mara zote akafanikiwa kwa 100%
➡Hakuna mlinda mlango aliyeokoa (saves) mara nyingi kwenye mchezo mmoja wa Kombe la Dunia mwaka huu kumzidi mlinda mlango Thibaut Courtois ambaye kwenye mchezo dhidi ya Brazil ameokoa mara 9.
➡N'Golo Kante ndiye mchezaji aliyekata umeme (interceptions) mara nyingi zaidi kuliko mchezaji yoyote kwenye Kombe la Dunia mwaka huu, amekata umeme mara 13 (kabla ya mchezo dhidi ya Uruguay)
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment