Uchambuzi; Kuelekea Chelsea vs Cardiff city (15-Septemba-2018) - Darajani 1905

Uchambuzi; Kuelekea Chelsea vs Cardiff city (15-Septemba-2018)

Share This

Mara baada ya Chelsea kumalizana dhidi ya Afc Bournemouth, zitapita siku 14 kabla ya Chelsea kucheza mchezo mwingine dhidi ya Cardiff city ambao msimu uliopita walikuwa ligi daraja la kwanza maarufu kama Championship.

Chelsea itakuwa nyumbani kwa mara nyengine tena ikishuka kumenyana dhidi ya Cardiff city ambao bila shaka watashuka wakiwa na nia ya kujionyesha sasa wamerudi kwenye ligi kuu tangu waliposhuka msimu wa 2013-2014.

Matokeo ya mchezo uliopita kwa Chelsea utakuwa na sehemu kubwa ya kuifanya ishuke kwenye mchezo huu ikiwa na hali fulani, kama itafanikiwa kushinda mchezo uliopita ambao ndio dhidi ya Bournenouth basi itawafanya wajiamini na kuwa na uwezo mkubwa wa kupata matokeo mazuri dhidi ya klabu hii ambao wao ndio walikuwa mabingwa wa ligi daraja la kwanza nchini Uingereza (Championships)

Tukirudi kwenye historia inaonyesha Cardiff city ilikuwa inamsumbua Chelsea haswa kwenye miaka hiyo wakati bado Chelsea ilikuwa haijajijenga ukiangalia mchezo wa kwanza kwa klabu hizo kumenyana ilikuwa mwaka 1921 tena kwenye michuano ya Kombe la FA ambapo Chelsea ilipoteza kwa magoli 2-1.

Lakini kutokana na kukosekana kwa klabu hiyo kwenye ligi kuu Uingereza ambapo ilishiriki msimu mmoja na ikashindwa kupambana mpaka ikashuka daraja kwenye msimu huohuo wa 2013-2014.

Katika michezo mitano ya mwisho, Chelsea imeshinda michezo mitatu na kutoa sare mchezo mmoja huku ikipoteza mchezo mmoja.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment