Nilikuletea habari hii leo kwamba klabu ya Chelsea inaweza kumpa mkataba mpya mlinda mlango nambari tatu, Eduardo mwenye miaka 35 ambaye hajawai kuichezea Chelsea mchezo wowote, hatimaye nyota huyo amepewa mkataba mpya wa mwaka mmoja lakini akitolewa kwa mkopo.
Chelsea imempa mlinda mlango huyo mwenye miaka 35 mkataba wa mwaka mmoja lakini pia ikimtoa kwa mkopo kwenye klabu ya Vitesse ya nchini Uholanzi.
Huyu ni mchezaji wa 26 wa Chelsea kujiunga kwa mkopo kwenye klabu hiyo huku siku kadhaa zilizopita walitoka kumsainisha mwengine kutoka Chelsea, Jake Clarke-Salter ambaye naye alijiunga kwa mkopo.
Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ana urafiki na mmiliki wa Vitesse, Leonid Slutsky na hivyo kufanya nyota wengi wa Chelsea kupelekwa kwa mkopo klabuni hapo.
Kwa umri wa Eduardo wa miaka 35, unazani kulikuwa na ulazima wa Chelsea kumpa mkataba mpya?
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment