Hazard ajiandaa kuachana na Chelsea - Darajani 1905

Hazard ajiandaa kuachana na Chelsea

Share This

Klabu ya nchini Uholanzi, VVV Venlo imetoa ripoti kwamba nyota wa kikosi cha vijana cha Chelsea, Kylian Hazard anajiandaa kufanya majaribio kwenye klabu hiyo kwa siku 10.

Nyota huyo ambaye ni mdogo wa Eden Hazard hajafanikiwa kuichezea mchezo wowote klabu ya wakubwa huku akitumika zaidi kwenye klabu za vijana za klabu hiyo.

Mwaka uliopita, baba mzazi wa kiungo huyo aliwai kukaririwa akisema wanajifikiria kumhamisha mtoto wao wakiamini klabu hiyo ni ngumu kuwaamini vijana na kuwapa nafasi.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment