Viongozi wa Chelsea wafanya mawasiliano na Maurizzio Sarri - Darajani 1905

Viongozi wa Chelsea wafanya mawasiliano na Maurizzio Sarri

Share This

Taarifa iliyoriporipotiwa na chombo cha habari nchini Italia, Corriere Dello Sport limeripoti kwamba klabu ya Chelsea imefikia sehemu nzuri katika usajili wake wa kumnasa kocha Maurizzio Sarri kutoka klabu ya Napoli.

Taarifa hiyo iliyoripotiwa inadai kwamba klabu hiyo imefanya mawasiliano na kocha huyo mwenye miaka 59 huku akipewa taarifa aanze safari ya kutoka nchini Italia mpaka nchini Uingereza ambapo huko atakutana na uongozi wa Chelsea.

Taarifa hiyo pia inazidi kudadavua kwamba usajili wa kocha huyo unaweza kutangazwa mwanzoni mwa wiki ijayo kama mambo yanayotarajiwa yakienda sawa.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment