Aliyewai kuwa kiongozi wa Chelsea akiwa anahusika na majukumu ya usajili, Michael Emenalo ambaye kwa sasa anatimiza majukumu hayo akiwa na klabu ya nchini Ufaransa, As Monaco amefanikiwa kumsajili kinda wa Chelsea, Jonathan Panzo.
Panzo mwenye miaka 17 ambaye amekuwa akitumika kwenye klabu za vijana za akademi ya Chelsea amekamilisha uhamisho huo wa moja kwa moja.
Klabu ya Chelsea kupitia tovuti yake imemtakia kheri nyota huyo ambayo aliiongoza timu yake ya taifa, Uingereza kushinda Kombe la Dunia kwa vijana mwaka 2017.
Emenalo aliyeandika barua ya kuomba kujiuzuru klabuni Chelsea huku mashabiki wengi wakimchukia haswa kutokana na mfumo wa usajili ni kama analipiza kisasi kwa kuwasajili nyota wa Chelsea.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment