Kombe la Dunia; Nyota 6 kati ya 8 wa Chelsea kushuka uwanjani leo - Darajani 1905

Kombe la Dunia; Nyota 6 kati ya 8 wa Chelsea kushuka uwanjani leo

Share This

Baada ya kupumzika siku mbili tukitenganisha michezo ya timu 16 bora na michezo ya robo fainali hatimaye ijumaa ya leo kunaendelea michuano ya Kombe la Dunia huku kwa upande wa nyota wa Chelsea watakaocheza leo ni nyota sita kati ya nyota nane waliofanikiwa kufudhu kucheza hatua hiyo ya robo fainali.

Uruguay vs Ufaransa
Mchezo wa mapema utakaochezwa saa 17:00 kwa saa za Afrika Mashariki utawashuhudia nyota wawili wa Chelsea kwa upande wa timu ya Ufaransa. Nyota hao ni pamoja na N'Golo Kante akiwa na mshambuliaji Olivier Giroud ambao watahitaji kuzisaidia timu zao zifudhu kucheza hatua inayofata ya nusu fainali.

Brazil vs Ubelgiji
Mchezo huu utaanza saa 21:00 kwa saa za Afrika Mashariki na utawakutanisha nyota wanne kwenye timu mbili tofauti.
Brazil; Willian Borges anaweza kutumika kwenye kikosi cha kwanza kwenye mchezo huu haswa kutokana na uwezo anaouonyesha katika kila mchezo huku kwenye mchezo uliopita alitoa pasi ya mwisho ya goli lililofungwa na Neymar na kuifanya Brazil ishinde 2-0 dhidi ya Mexico

Ubelgiji;
Eden Hazard ambaye ndiye nahodha mkuu wa kikosi cha Ubelgiji amesifiwa na kocha wake Roberto Martinez ambaye amedai kukoshwa na uwezo na uongozi anaounyesha nyota huyo, nyota wengine wa Chelsea ni pamoja na mlinda mlango nambari moja kwa Chelsea na Ubelgiji pia, Thibaut Courtois pamoja na mshambuliaji Michy Batshuayi.

Nyota wawili waliobaki kwenye orodha hiyo ni Gary Cahill pamoja na Ruben Loftus-Cheek ambao wataiongoza Uingereza kesho jumamosi ya tarehe 7-Julai kucheza dhidi ya Sweden kwenye hatua ya robo fainali.

Kupata habari zote kuhusu Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment