Toka amefika klabuni Chelsea hajafanikiwa kupata nafasi ya kuichezea klabu hiyo akitumika tu kama mlinda mlango nambari tatu huku akitoa upinzani kwa makipa Thibaut Courtois na Willy Caballero au Asmir Begovic kabla ya kuondoka.
Ni mchezaji raia wa Ureno, Eduardo dos Reis Carvalho anatajwa kuweza kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja wa kuendelea kusalia kabuni Chelsea licha ya kutopata nafasi ya kucheza.
Mlinda mlango huyo raia wa Ureno aliyekuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ureno kilishoshinda michuano ya Ulaya kwa mwaka 2016 anatajwa na chanzo kimoja kinachoaminika kwamba yupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kusalia Chelsea kwa msimu mwengine.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment