Chelsea kucheza kamari, yajiandaa kuvunja rekodi kwa Lingard - Darajani 1905

Chelsea kucheza kamari, yajiandaa kuvunja rekodi kwa Lingard

Share This

Gazeti la Dailystar la nchini Uingereza limekuja na habari mpya, habari inayoweza kumfanya kila mwana Chelsea akashangazwa.

Gazeti hilo limechapisha habari kwamba klabu ya Chelsea inaweza ikaweka mezani paundi milioni 80 ili kumnasa mchezaji wa klabu ya Manchester united, Jesse Lingard ambaye amekuwa moja ya sababu ya kufanikiwa kwa timu yake ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko nchini Urusi

Lingard mwenye miaka 25 ameagiza kulipwa mshahara wa paundi 150,000 kwa wiki kwenye klabu yake ya Man utd na kama ikitokea akakataa kuendelea kuichezea klabu hiyo basi Chelsea ni moja ya klabu zinazomtamani.

Jambo nalosema litawashangaza wengi katika usajili huu ni kutokana na Chelsea kutokuwa na kawaida ya kununua wachezaji kutoka Man utd na hata kama ikiwasajili huwa wanafanya vibaya ambapo mchezaji wa mwisho kusajiliwa alikuwa ni Juan Sebastian Veron ambaye alitoka Man utd na kuja Chelsea mwaka 2003 na alifanya vibaya mpaka akacheza michezo 7 tu akiwa mchezaji wa Chelsea na baadae akapelekwa kwa mkopo kabla ya kuuzwa. Mwengine alikuwa mlinda mlango Bosnich aliyesajiliwa mwaka 2001 lakini aliichezea Chelsea michezo 5 tu.

Hapo hatumuweki Radamel Falcao maana Chelsea ilimchukua kwa mkopo akitokea AS Monaco sio Man utd maana hakuwa mchezaji wao.

Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905

No comments:

Post a Comment