Tarehe mosi mwezi Septemba, Chelsea itakuwa nyumbani kwa mara nyengine ikicheza mchezo wa nne wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Afc Bournemouth.
Mchezo huu utakuja siku 7 baada ya Chelsea kukutana na kibarua kigumu kutoka kwa Newcastle united itakayokuwa nyumbani kwake pale St. James Park. Kama Chelsea itaendeleza matokeo mabaya kwenye uwanja huo basi nina hakika itarudi kumenyana dhidi ya Afc Bournemouth huku ikiwa na hasira, haswa hasira hizo zitaongezeka kutokana na Chelsea kuwa na kumbukumbu ya mchezo iliopoteza ikiwa nyumbani kwa msimu uliomalizika ambapo Chelsea ilipoteza ikiwa nyumbani kwa magoli 0-3.
Nyota wa zamani wa Chelsea, Nathan Ake anaweza kuzidi kuukamia mchezo huo kama akipewa nafasi akitaka kuionyesha Chelsea kwamba ilikosea kuachana nae ikimuuza kwa usajili wa jumla kwenda kwenye klabu hiyo aliyoitumikia kwa mkopo hapo kabla ya kutia saini akiwa kama mchezaji wao.
Lakini Chelsea nayo itataka kulipiza kisasi kwa kuionyesha kwamba mkubwa ni mkubwa tu.
Kihistoria inasema klabu hizi hazina historia kubwa kwenye kukutana uso kwa uso ambapo zilikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1988 wakati Bournemouth akiwa kwao katika michuano ya ligi daraja la pili ambayo kwa sasa ndio inaitwa Championship (ligi kuu kipindi iko ilikuwa ikiitwa ligi daraja la kwanza) na Bournemouth aliondoka na ushindi wa goli 1-0 lakini katika michezo mitano ya mwisho, Chelsea imeshinda michezo minne huku ikipoteza mchezo mmoja.
Kiujumla klabu hizo zikikutana hakujawai kumalizika kwa sare ambapo kwenye michezo 12 ambayo klabu hizo zimekutana, Chelsea imeshinda michezo 9 huku ikipoteza michezo mitatu.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
Uchambuzi; Kuelekea Chelsea vs Afc Bournemouth (1-Septemba-2018)
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment