Kocha wa klabu ya Manchester united, Jose Mourinho anatajwa kuendelea kumfukuzia winga na nyota wa klabu ya Chelsea, Willian Borges ili ajiunge na klabu yake katika kipindi iki cha usajili wa dirisha kubwa.
Mourinho ambaye aliwai kuifundisha Chelsea na yeye ndiye alimsajili nyota huyo kumleta klabuni Chelsea anatajwa kuandaa dau la paundi milioni 60 ili kumnasa nyota huyo ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni kutokana na timu yake ya Brazil kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwenye hatua ya robo fainali.
Chelsea inatajwa kuhitaji paundi milioni 72 kutoka kwa Barcelona ambao wao walitoa ofa ya paundi milioni 50 ili kumsajili nyota huyo mwenye miaka 29 lakini Chelsea ikakataa kumuuza kwa dau hilo na sasa inatajwa kuandaliwa paundi milioni 60 ili kumuuza kwa Man utd klabu ambayo mashabiki wengi hatutaki aende kutokana na kuwa mshindani wetu kwenye ligi kuu Uingereza.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment