Jana jumapili ilikuwa siku ya mwisho kwa nyota wa Chelsea ambao hawakuungana na timu zao za taifa kwenye michuano ya Kombe la Dunia kurejea klabuni ili kujiandaa na michezo ya kirafiki kuelekea msimu mpya wa 2018-2019.
Nyota hao wamefika klabuni hii leo wakiendelea na mazoezi waliyoyaanza toka jumamosi ya tarehe 7-Julai mwaka huu lakini kubwa likiwa ni ujio wa kocha Antonio Conte licha ya kocha huyo kuripotiwa mara kadhaa kwamba hatoendelea kuifundisha klabu hiyo kwa msimu wake wa mwisho kwenye mkataba wake klabuni Chelsea.
Kocha huyo alionekana siku hiyo ya jumamosi akiwa uwanjani pamoja na makocha wa benchi lake la ufundi lakini taarifa zikaenezwa kwamba kocha huyo ataanza majukumu yake pamoja na kikosi siku ya jumatatu.
Na hatimaye jumatatu imefika na kocha huyo ameonekana pamoja na nyota wa Chelsea wakiwa mazoezini na hii imeleta tafsiri mpya huku yakiwa na maswali kibao.
Je Conte ataendelea kuifundisha Chelsea kwa msimu mwengine? Je vipi kuhusu Maurizzio Sarri ataendelea kutakiwa na Chelsea? Mahusiano kati ya Conte na bodi ya Chelsea ni mazuri, sio kama ilivyokuwa inaripotiwa?
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment