Bila shaka wote tunakubaliana kwamba nusu fainali ya Ufaransa dhidi ya Ubelgiji ndiyo nusu fainali inayosubiriwa kwa hamu zaidi huko nchini Urusi kwenye michuano ya Kombe la Dunia itakayochezwa hapo kesho.
Kuelekea kwenye nusu fainali hiyo itakayowakutanisha nyota watano kutoka Chelsea ambao ni N'Golo Kante na Olivier Giroud kwa upande wa Ufaransa wakati kwa upande wa Ubelgiji kutakuwa na Eden Hazard, Michy Batshuayi na mlinda mlango Thibaut Courtois nyota Eden Hazard ametoa neno kuhusu kiungo wa Ufaransa, N'Golo Kante ambaye anatajwa kuwa kiungo mkabaji bora kwa sasa.
"Kante ni mchezaji bora zaidi kwa nafasi yake, ni mchezaji anayecheza kwa ubora zaidi na naamini ukicheza nae basi una 95% za kushinda mchezo" alisema Hazard ambaye mpaka sasa ameshaichezea Ubelgiji michezo minne huku akiifungia magoli 2 na kutoa pasi za mwisho 2 kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia.
Je nani ataibuka kidedea kwenye michuano hiyo? usisahau kuandika maoni (comment) yako hapa chini na kuwasambazia (share) wengine
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment