JE MARCOS ALONSO NA BAKAYOKO KUCHEZA DHIDI YA BARCELONA? - Darajani 1905

JE MARCOS ALONSO NA BAKAYOKO KUCHEZA DHIDI YA BARCELONA?

Share This
Jana kocha Antonio Conte aliiongoza vyema Chelsea kupata ushindi wake wapili mfululizo mara baada ya kutoka kwenye dimbwi baya la kupoteza michezo miwili mfululizo na kutokuwa na matokeo mazuri. Kwa ushindi huo wa jana ambapo Chelsea iliibamiza Hull city magoli 4-0 na kufanikiwa kusonga mbele kwenye kombe hilo la FA na sasa kufikia hatua ya robo fainali, kocha Antonio Conte aliulizwa juu ya maendelea ya wachezaji wa Chelsea, Marcos Alonso pamoja na tiemoue Bakayoko kama wataweza kujumuika na timu kuelekea kwenye mchezo wa jumanne ambapo Chelsea itakuwa nyumbani kupambana dhidi ya Barcelona katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya.

"Ndiyo, Marcos Alonso atakuwa tayari kukabiliana katika mchezo huo. Kwa Bakayoko sidhani kama atakuwa sawa kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo, lakini kwa Marcos Alonso, nna uhakika atakuwa sawa zaidi kucheza kwenye mchezo huo" alisema Antonio Conte alipoulizwa juu ya nyota hao kama watakuwepo kwenye kikosi cha Chelsea siku hiyo.

Marcos Alonso hajatumika katika michezo mingi mfululizo, akikosekana kwenye michezo dhidi ya afc Bournemouth, Watford, West Bromwich na mchezo wa jana dhidi ya Hull city huku kukiwa hakuna taarifa za moja kwa moja kuwa nyota huyo ni majeruhi.

Darajani 1905 inaona kukosekana kwa nyota huyo katika michezo minneb mfululizo ni kutokana na kupewa muda zaidi wa kupumzika ili kuwa sawa kupambana katika mchezo huu wa klabu bingwa Ulaya ambao kiukweli ni mchezo mgumu, na Chelsea inahitaji ushindi ili kuweza kusogea kwenye hatua nyengine. Kama una kumbukumbu vizuri, mara baada ya mchezo ambao Chelsea ilipoteza mbele ya Watford, wachezaji wa Chelsea walipewa siku tatu za kupumzika na kurudi mazoezini siku ya ijumaa ambapo kwa njia hiyo, kocha Antonio Conte alipoulizwa alisema ni njia nzuri kwa klabu kupumzika na kujiweka sawa kutokana na kucheza michezo mingi mfululizo bila kupumzika. Na toka Chelsea irudi kwenye mapumziko hayo, wachezaji wamekuwa na hali kubwa ya ushindi na morali ya timu imekuwa sawa. Ikifunga magoli 7 katika michezo miwili huku haijaruhusu kufungwa goli lolote, lakini pia ikishinda michezo yote, dhidi ya West Bromwich na dhidi ya Hull city.

No comments:

Post a Comment