GWIJI WA SOKA AMUOMBA RADHI TIEMOUE BAKAYOKO - Darajani 1905

GWIJI WA SOKA AMUOMBA RADHI TIEMOUE BAKAYOKO

Share This
Gwiji wa soka, Phil Brown ambaye aliyewai kutamba na klabu ya Hull city kama kocha wa klabu hiyo ambayo jana ilipambana na Chelsea kwenye mchezo wa raundi ya tanoya kombe la FA na klabu hiyo kupokea kipigo cha mabao 4-0 katika uwanja wa Stamford Bridge amemuomba msamaha kiungo wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko juu ya maneno aliyotamka juu yake wakati gwiji huyo alipohojiwa na jarida la Talksport.

Gwiji huyo ambaye aliwai kutamba kama mchezaji kwenye vilabu vya Derby County na Preston North End alikaririwa na gazeti hilo wiki iliyopita wakati klabu yake hiyo ilipokuwa inajiandaa kumenyana na Chelsea akitoa maneno ambayo hayakuonekana kama ni mazuri haswa kuongea kwenye vyombo vya habari akiongea kumlenga Bakayoko ambaye mchezo wake wa mwisho alicheza na kupewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Watford ambapo Chelsea ilipoteza kwa magoli 4-1.

"Kiukweli napenda kuomba radhi kwa maneno niliyotumia maana najua yamesababisha kutokueleweka nilipoyaongea katika Talksport wiki iliyopita. Hayakuwa maneno mazuri, na yalishambulia na kutoleta maana nzuri. Kiukweli nimeelewa kuwa hayakuwa maneno mazuri na kiasi gani yalionyesha ubaya" alisema gwiji huyo.

Tiemoue Bakayoko kwa sasa anauguza majeruhi yanayomfanya kuukosa mchezo dhidi ya Barcelona, ambapo hiyo imeelezwa na kocha Antonio Conte ambapo atakosekana yeye wakati kwa upande wa Marcos Alonso atakuwepo kwenye mchezo huo.

No comments:

Post a Comment