MCHEZAJI WA BARCA AIPA CHELSEA SILAHA ILI KUWA BORA - Darajani 1905

MCHEZAJI WA BARCA AIPA CHELSEA SILAHA ILI KUWA BORA

Share This
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amekuwa akitajwa kuondoka klabuni hapo ifikapo mwisho wa msimu huu, huku akihusishwa kutaka kurudi nchini Italia ambapo huko ndiko kwao na ameanzia kufundisha soka akiwa nchini huko na kupata mafanikio makubwa. Kwa tetesi hizo zakocha huyo kuondoka kumekuwa kukimfanya kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique kutajwa kwa karibu kutua klabuni hapo.

Mara baada ya kocha huyo kutajwa kutakiwa na chelsea, nyota na mlinzi wa klabu ya Barcelona, Thomas Vermaelen anaogopa Chelsea kumnasa kocha huyo raia wa Hispania akidhani kama kocha huyo akitua Chelsea, basi Chelsea itakuwa katika ubora wa hali ya juu.

Nyota huyo alipohojiwa juu ya koha huyo ambaye aliwai kumfundisha klabuni Barcelona, amesema "Nilikuwa sipati nafasi mara nyigi kucheza chini yake, lakini uhusiano wake na wachezaji ni mzuri. Jinsi anavyoongea na wachezaji ni aina ya upekee. Anajua kumfanya mchezaji ajihisi vizuri na kujihisi kuwa bora. Kama ukiniuliza nikutajie makocha bora niliowai kufundishwa nao, sintoacha kumtaja"

Alipoulizwa kama Luis Enrique ataweza kuipa Chelsea ukubwa kama alivyofanya kocha wa zamani wa Barcelona ambaye kwa sasa anafanya vizuri na klabu ya Mama site (Man city), nyota huyo alisema "Nadhani atafanya ivo. nadhani atafanya makubwa kama haya tunayoona anayafanya Pep Guardiola akiwa na Man city. Itamchukua muda kidogo lakini naamini atafanikiwa"

Vermaelen aliwai kuichezea klabu ya Arsenyani (Arsenal) kabla hajaungana na Barcelona, na ametumia muda mwingi klabuni huko kuwa kama mchezaji wa akiba au akitumia kuuguza majeruhi yake aliyokuwa nayo tangu anatoka Uingereza. Na jumanne anaweza akawemo kwenye kikosi cha Barcelona kitakachomemenyana dhidi ya Chelsea katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.


No comments:

Post a Comment