MARCO ASENSIO KUTUA CHELSEA? MSIKIE ANACHOKISEMA - Darajani 1905

MARCO ASENSIO KUTUA CHELSEA? MSIKIE ANACHOKISEMA

Share This
Chelsea imekuwa ikitajwa kuvutiwa na nyota wa klabu ya nchini Hispania, Marco Asensio ambaye anaichezea klabu ya Real Madrid, huku kukiwa na taarifa kuwa tajiri wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich alikuwa akipendezwa na Cristiano Ronaldo kabla ya baadae washauri wake kumshauri ni bora akamchukua Marco Asensio ambaye ana muda mrefu wa kucheza soka lake ambapo kwa sasa ana miaka 22, ni tofauti na Ronaldo mwenye miaka 33.

Lakini pia kwa upande wa tajiri wa Real madrid inadaiwa yupo tayari kumtumia nyota wake huyo ili kufanya mabadilishano na Chelsea ili wao wamnase Eden Hazard, huku kukiwa pia kuna taarifa kuwa nyota huyo (Asensio) alimwambia rais huyo kama Eden hazard akisajiliwa na Real madrid basi naye ataondoka klabuni hapo.

Sasa tena na leo kuna taarifa mpya zimetoka, ambapo nyota huyo kwa mdomo wake mwenewe amesema hatazamii kuondoka klabuni Real Madrid na tazamio lake kubwa klabuni hapo ni kugombania nafasi katika kikosi cha kwanza na hata kama anakosa nafasi hiyo ataendelea kubaki ili kushindania nafasi hiyo.

"Kufika na kuichezea klabu kubwa duniani kama hii ambayo ina mshabiki wengi duniani ni jambo kubwa kwangu. Mchezo wangu wa kwanza ulikuwa katika fainali na nikafanikiwa kufunga  na nikafanikiwa kushinda taji langu la kwanza"

"Katika michezo yangu nayopata nafasi yote najitahidi kutimiza nalotakiwa kulifanya na nimefika Madrid kwa lengo la kufunga na kuendelea kuwa hapa, na sio kuondoka" alisema winga huyo.

Chelsea ilishawai kutajwa kumtaka nyota huyo kwa dau la paundi milioni 120, hiyo ikiwa bila kufanyika mabadilishano na Eden Hazard.

No comments:

Post a Comment