LOFTUS-CHEEK KUREJEA UWANJANI - Darajani 1905

LOFTUS-CHEEK KUREJEA UWANJANI

Share This
Nyota wa Chelsea aliyeko kwa mkopo klabuni Crystal palace, Ruben Loftus-Cheek anaweza akarejea uwanjani muda wowote kuanzia sasa mara baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu na kumfanya kukosa michezo yote ambayo klabu yake ya mkopo imecheza toka kuingia mwaka 2018 ambapo amekuwa nje toka mwaka jana mwezi Desemba tarehe 28.

Kocha wake kwenye klabu ya mkopo, Roy Hodgson alitoa ripoti juu ya majeruhi na kurejea uwanjani kwa nyota huyo, "Anaweza akaondoka Chelsea na kuungana nasi kati ya alhamisi au ijumaa na kuweza kujuuika nasi katika mchezo wa mwisho wa wiki. huo ndio mpango uliopo kwa sasa."

"Habari njema ni kwamba, majeraha aliyoyapata ambapo aliumia kwa ndani kunaonekana kuimarika na kuwa sawa na kuweza kurejea uwanjani hivi karibuni" alisema kocha huyo ambaye jana alishinda tunzo ya kocha bora wa mwaka 2018 katika tunzo za jiji la London (London Football Awards 2018)

Nyota huyo raia wa Uingereza alirudi klabuni Chelsea kwa ajili ya matibabu ambapo alikuwa kwenye uangalizi wa madaktari wa Chelsea pamoja na ushirikiano na madaktari wa Crystal Palace, na kwa maana hiyo huenda akaungana na kikosi cha timu ya taifa cha Uingereza kushiriki michuano ya kombe la dunia huko nchini Urusi ambapo mwanzoni kulikuwa na wasiwasi kuwa labda majeraha yangemweka nje.

No comments:

Post a Comment