Vigogo barani Ulaya vyaanza kumnyemelea Hudson-Odoi - Darajani 1905

Vigogo barani Ulaya vyaanza kumnyemelea Hudson-Odoi

Share This

Moja kati ya wachezaji makinda wanaotikisa nchini Uingereza kwa sasa ni pamoja na nyota wa kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 18 wa Chelsea maarufu kama Chelsea U18s, Callum Hudson-Odoi ambaye amekuwa msingi imara kwenye mafanikio ya klabu hiyo ya vijana iliyochini ya kocha Jody Morris ambapo kwa msimu huu tayari wameshashinda mataji manne na kufanikiwa kukata tiketi ya kucheza klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao.

Lakini ukubwa wa nyota huyo raia wa Uingereza kwenye uchezaji wake unatajwa kuzitoa udenda klabu vigogo barani Ulaya na sasa klabu za Barcelona, Real Madrid na Juventus zinatajwa kuvutiwa na nyota huyo na sasa zimepanga kuifata Chelsea ili kumsajili.

Nyota huyo mwenye miaka 17 kwa sasa ambaye ana uwezo mkubwa wa kucheza kama winga na mshambuliaji amefanikiwa kuichezea kwa mara ya kwanza kikosi cha Chelsea FC michezo mitatu ndani ya msimu huu anatajwa kuwa moja ya hazina kubwa na ya muhimu kwa Chelsea ambapo alijiunga na akademi hiyo ya Chelsea toka akiwa na miaka 8.

Kocha wa kikosi cha Chelsea U18s, Jody Morris alitoa ushauri juu ya mchezaji huyo kwa kocha Antonio Conte na klabu kwa ujumla, kuusoma ushauri huo, bonyeza hapa
*********
Bila kusahau zimesalia siku 12 kabla ya mashabiki wa Chelsea na wapenzi wote wa soka kukutana pale Hospitali ya serikali ya Temeke jijini Dar es Salaam ili kuifanya jamii yetu ifaidike kwa kupenda kwetu soka ambapo tutachangia damu kwa hiyari
#CharityForTheBlues

No comments:

Post a Comment