Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea imefanikiwa kutwaa taji la kombe la FA mara baada ya kuibamiza klabu ya soka ya wanawake ya Arsenal kwa mabao 3-1 kwenye uwanja wa Wembley.
Shukrani kwa magoli mawili ya nyota Ramona Bachmann pamoja na goli moja la nyota Fran Kirby na kutimiza ushindi huo wa magoli 3-1 na kuifanya klabu hiyo maarufu kama Chelsea Ladies kushinda taji hilo.
Rekodi iliyowekwa katika fainali hiyo ni ya nyota wake ambae ni nahodha wa kikosi hicho cha Chelsea Ladies, Katie Chapmann ambaye alitimiza taji la kumi akiwa ndiye mchezaji pekee kwa soka la wanawake kushinda mataji kumi.
Hongereni madada mkiongozwa vyema na kocha makini, Emma Hayes
*********
Bila kusahau zimesalia siku 13 kabla ya mashabiki wa Chelsea na wapenzi wote wa soka kukutana pale Hospitali ya serikali ya Temeke jijini Dar es Salaam ili kuifanya jamii yetu ifaidike kwa kupenda kwetu soka ambapo tutachangia damu kwa hiyari
#CharityForTheBlues
No comments:
Post a Comment