Giroud kushangilia pamoja na Luiz, je kulimaanisha nini? - Darajani 1905

Giroud kushangilia pamoja na Luiz, je kulimaanisha nini?

Share This

Victor Moses akitumia ufundi wake mkubwa kwa kupiga krosi murua iliyomkuta vyema Olivier Giroud ambaye aliutumbukiza mpira wavuni kwa kutumia kichwa chake. Mfaransa huyo akashangilia goli hilo kwa kumfata mchezaji mwenzake, David Luiz ambaye hakuwa kwenye benchi kama mchezaji wa akiba ila alikuwa kama mmoja wa watu maalumu kwa Chelsea akiwa pamoja na wachezaji wa Chelsea wasiojumuishwa na kikosi cha mchezo wa leo ambao ni Danny Drinkwater sambamba na Ethan Ampadu.

Giroud alimfata David Luiz na kumkumbatia kama sehemu ya ushangiliaji wa goli hilo. Jambo hilo limezua mjadala mkubwa haswa kuwepo na tetesi za Luiz kutokua sawa na kocha wake Antonio Conte.

Nyota David Luiz ambaye ni raia wa Brazil ameutumia mtandao wa Instagram kuonyesha hisia zake haswa kutokana na mfaransa huyo kushangilia pamoja nae.

"Asante Bwana! Urafiki mzuri Mungu kanipatia mwaka huu. Asante sana rafiki yangu 'Oli, Oli'! Ni wakati wa furaha!
#fightinguntiltheend"

Huu ni uhusiano mzuri unaonekana kuibuka kati ya nyota hawa wawili lakini uhusiano huu au ushangiliaji huu umetafsiriwa na baadhi ya mashabiki wa Chelsea kuwa nyota huyo anatoa ujumbe kwa kocha wa Chelsea, Antonio Conte kuwa anahitaji kumrejesha nyota huyo kikosini. Lakini nani anajua? subiri nitajaribu kutafuta mahojiano aliyofanyiwa nyota huyo mwenye miaka 31 kwa sasa kwamba ni nini alikimaanisha juu ya ushangiliaji wake huo.
*********
Bila kusahau zimesalia siku 13 kabla ya mashabiki wa Chelsea na wapenzi wote wa soka kukutana pale Hospitali ya serikali ya Temeke jijini Dar es Salaam ili kuifanya jamii yetu ifaidike kwa kupenda kwetu soka ambapo tutachangia damu kwa hiyari
#CharityForTheBlues

No comments:

Post a Comment