Sijui nianze kusema nini, asikwambie mtu raha ya kupenda, haswa ukakipenda kizuri alafu iko kizuri kikawa kinajua kupendeka. Asante Chelsea kwa kunifanya nijivunie kukupenda, asante Giroud kwa kunifanya mtaani nitembee kitambi mbele. Ningekuwa yule jamaa mweupe wa pale msimbazi basi leo ningewafata wale wazee wa ule mziki wa dansi wanipigie tena ule wimbo wa kitambaa cheupe.
Tiemoue Bakayoko aliyewafanya wengi waamini hastahili kuwepo Darajani anapiga pasi ndefu kwa mtoto wa mchungaji, Victor Moses ambaye anadhirisha mapenzi yake makubwa kwa Chelsea licha ya kusemwa sana pindi aliposajiliwa akikosa nafasi na kuishia kutolewa kwa mkopo na wengi wakimsema kwamba aondoke Chelsea akimpindua vyema mlinzi wa Liverpumba amna namaanisha Liverpool na kuipiga krosi moja murua inayoweza kutibu magonjwa yote sugu na kama kawaida yake Olivier Shindika Giroud akautumbukiza mpira nyavuni huku mlinda mlango akibaki akishangaa na asielewe nini cha kufanya.
'This is Chelsea' goli hilo pekee lililopatikana katika kipindi cha kwanza linadumu mpaka pale mwamuzi Anthony apulize filimbi ili kuumaliza mpira.
Chelsea sasa inafikisha alama 69 huku ikiachwa alama mbili na Tottenham inayoshika nafasi ya nne ikiwa na alama 71 na Liverpool inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na alama 72 lakini ikiwa imebakiza mchezo mmoja ili ligi kuu nchini Uingereza imalizike wakati kwa upande wa Chelsea na Tottenham zote zimebakiza michezo miwili kila mmoja.
*********
Bila kusahau zimesalia siku 13 kabla ya mashabiki wa Chelsea na wapenzi wote wa soka kukutana pale Hospitali ya serikali ya Temeke jijini Dar es Salaam ili kuifanya jamii yetu ifaidike kwa kupenda kwetu soka ambapo tutachangia damu kwa hiyari
#CharityForTheBlues
No comments:
Post a Comment