Chelsea itacheza mchezo wake wa mwisho kwa msimu huu wa 2017-2018 hapo kesho ambapo itashuka tena kwenye uwanja wa Wembley unaopatikana jijini London ili kucheza mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la FA dhidi ya Manchester united.
Kuelekea kwenye mchezo huo mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud ambaye tangu acheze kwenye uwanja huo wa Wembley akiwa na Arsenal na hata aliposajiliwa na Chelsea na kuichezea mchezo mmoja wa nusu fainali ya michuano hiyo hajawai kushuhudia timu yake ikipoteza amefichua siri kuwa wakati anatua Chelsea alichukiwa sana na wachezaji wenzake klabuni hapo.
"Wakati nafika hapa na kukutana na wachezaji wenzangu, walinikasirikia sana. Hawakupenda mi nitue Chelsea. Lakini hilo halikunizoofisha maana nilisema mimi ni bora na nitaendeleza rekodi yangu ya kutokupoteza nikiwa Wembley, na naamini hilo litaenda kutimia hapo kesho" alisema mfaransa huyo ambaye alitua Chelsea kwa dau la paundi milioni 18.
Nyota huyo hakutegemewa kutua Chelsea wakati klabu hiyo ikisaka saini ya mshambuliaji wa kuweza kuisaidia klabu na kumpa changamoto mshambuliaji chaguo la kwanza, Alvaro Morata ambaye anaonekana kutokua vizuri kwenye safu ya ushambuliaji.
No comments:
Post a Comment