Chelsea yakubali kumuuza Willian - Darajani 1905

Chelsea yakubali kumuuza Willian

Share This

Chanzo cha habari cha nchini Italia maarufu kama Tuttosport kimeripoti habari kwamba Chelsea imekubali kumuuza winga wake Willian Borges da Silva ili ajiunge na klabu ya Manchester united inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho.

Dau la paundi milioni 66 linatajwa kuifanya Chelsea kukubali kumuuza mbrazil huyo kwenye klabu hiyo ya jijini Manchester huku ikikataa dau kama hilo la paundi milioni 66 kutoka kwa Barcelona ambao wamejaribu mara tatu kumnasa nyota huyo mwenye miaka 29.

No comments:

Post a Comment