Everton yafunga milango kwa mrithi wa Courtois klabuni Chelsea - Darajani 1905

Everton yafunga milango kwa mrithi wa Courtois klabuni Chelsea

Share This

Klabu ya Chelsea inahofia kumpoteza mlinda mlango wake nambari moja, Thibaut Courtois ambaye anatajwa kutakiwa na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ambako huko ndipo alipo kwasasa akiwa mapumzikoni mara baada ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia. Amefika nchini humo kukutana na familia yake ambayo amekuwa nayo mbali kwa muda mrefu.

Kwa taarifa zilizopo zinadai klabu hiyo ya Chelsea imepanga kumsajili mlinda mlango Jordan Pickford kama ikishindwa kumzuia Courtois anayetamani kuungana na familia yake nchini Hispania.

Lakini klabu ya Everton ambayo ndiyo anaitumikia Pickford imedai haipo tayari kumpoteza mlinda mlango wao ambaye pia ndiye nambari moja kwa timu yake ya taifa ya Uingereza.

Chelsea inadai kumtaka mlinda mlango huyo aliyekuwa msaada mkubwa kwa timu yake ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya Kombe la Dunia ambapo walifanikiwa kumaliza hatua ya nusu fainali.

No comments:

Post a Comment