M/Kirafiki; Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Inter Milan - Darajani 1905

M/Kirafiki; Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Inter Milan

Share This

Usiku wa leo kutachezwa mchezo mwengine wa kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa 2018-2019 ambapo Chelsea itashuka uwanjani kucheza dhidi ya Inter Milan huko nchini Ufaransa kwenye jiji la Nice.

Kuelekea kwenye mchezo huo kama ilivyoada hapa nakuletea habari muhimu unazopaswa kuzijua kuelekea kwenye mchezo huo utakaochezwa saa 21:05 kwa saa za Afrika Mashariki.

Chelsea;
Nyota walioshiriki Kombe la Dunia ambao ni kama N'Golo Kante, Olivier Giroud, Eden Hazard na Thibaut Courtois pamoja na wale waliorejea klabuni wakitokea mapumzikoni ambao nao pia walishiriki michuano hiyo ambao ni kama Cesar Azpilicueta, Willy Caballero na Andreas Christensen nao wataukosa mchezo huu akiwemo pia mlinda mlango mpya aliyesajiliwa siku mbili zilizopita, Robert Green hatoshiriki mchezo huu kutokana na kutojumuishwa katika kikosi kile cha wachezaji 25 watakaoshiriki michezo ya kirafiki.

Nyota wa Chelsea watakaoingoza leo klabu hiyo ni pamoja na David Luiz,Jorginho, Cesc Fabregas, Pedro na Alvaro Morata huku Kurt Zouma akikosekana kutokana na majeruhi aliyoyapata.

Chelsea inahitaji ushindi katika mchezo wa leo ili kuondoka mbabe katika mchezo wake wa pili wa kirafiki huku mchezo wa kwanza uliisha kwa wababe hao wa London kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Perth Glory.

Inter Milan
Klabu kutoka nchini Italia itashuka kwenye mchezo huu huku ikiwa tayari imeshacheza michezo minne ya kirafiki. Imeondoka na ushindi katika mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja huku ikitoa sare katika michezo miwili.

Muda;
Saa 09:05 Usiku (Saa 21:05) kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment