Klabu ya Chelsea imetajwa moja ya klabu zilizofanya mawasiliano ili kumnasa nyota wa klabu ya Napoli ya nchini Italia, Jorginho ambaye anatajwa kufukuziwa pia na klabu za Uingereza.
Wakala wa nyota huyo alifanyiwa mahojiano na chombo cha habari cha nchini Italia ambapo alidai kwa sasa yupo nchini Brazil lakini hajapokea mawasiliano yoyote kutoka kwa klabu anayoichezea nyota huyo kama kuna mipango ya kuongeza mkataba na badala yake amekua akipokea simu kutoka kwa klabu za Uingereza ikiwamo Chelsea.
Jorginho mwenye miaka 26 ambaye kiasili ni mzaliwa wa Brazil ambaye anaichezea timu ya taifa ya Italia akifanana na nyota wa Chelsea, Emerson Palmieri ambaye naye ni mzaliwa wa Brazil ingawa anaitumikia timu ya taifa ya Italia.
No comments:
Post a Comment