Nyota wa Chelsea awataja Diego Costa na Matic kwenye kuyumba kwa Chelsea - Darajani 1905

Nyota wa Chelsea awataja Diego Costa na Matic kwenye kuyumba kwa Chelsea

Share This
Moja kati ya nyota waliowai kupita klabuni Chelsea ni pamoja na mlinzi wa kushoto Wayne Bridge amefanyiwa mahojiano na kuulizwa juu ya Chelsea kuwa na msimu mbaya ambapo imeshindwa kutetea taji lake la ligi kuu huku ikimaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu na kushindwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa kwa msimu ujao.
Nyota huyo raia wa Uingereza alisema kuporomoka kwa Chelsea kumetokana na kukosekana mtu anayeweza kuwa kama kiongozi kama ilivyokua msimu uliopita wakati gwiji John Terry alipokua klabuni hapo huku akiachana na klabu hiyo mara baada ya msimu kuisha na sasa anaitumikia klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi daraja la kwanza Uingereza maarufu kama Championship lakini pia ikimkosa Diego Costa ambaye alikuwa moja ya wachezaji wenye sauti klabuni hapo ila pia ikikosa huduma ya Nemanja Matic ambaye kwa sasa anaichezea Man utd.
"Nikikumbuka kipindi kile nikiwa hapa, nakumbuka timu iliyojaa wachezaji wenye sifa ya uongozi. Kulikua na Michael Ballack, Claude Makelele, Didier Drogba, John Terry, Frank Lampard, Ashley Cole na wengine wengi"
"Lakini kwa sasa mambo ni tofauti, baada ya nahodha aliyedumu kwa muda mrefu, John Terry kuondoka Chelsea na kiungo muhimu Nemanja Matic pamoja na mshambuliaji mkali Diego Costa ambao wote wameondoka Chelsea kwenye usajili wa kiangazi. Naamini kukosekana kwao kunaifanya Chelsea kuwa na tatizo la mtu anayeweza kuwa kiongozi kwa asilimia 100. Nikiiangalia Chelsea ya sasa siioni Chelsea yenye wingi wa viongozi. Naamini hilo wanabidi walitibu kama wanataka kuwa timu ya kugombania mataji."
"Kuwasajili wachezaji wakubwa na wenye majina makubwa sio suluhu ya Chelsea kufanya vizuri. Ila inahitaji ikubali kutumia gharama zozote ili kuwaleta wachezaji wenye sifa ya uongozi, hata kwa gharama mara mbili zaidi" alisema nyota huyo wa zamani
Chelsea itacheza mchezo wake wa mwisho hapo kesho dhidi ya Manchester united katika fainali ya kombe la FA ambapo hiyo ndiyo nafasi pekee kwa klabu hiyo kuweza kushinda taji msimu huu.

No comments:

Post a Comment