Mwaka 1998 klabu ya Chelsea ilifanikiwa kutwaa taji lake la kwanza la barani Ulaya maarufu kama UEFA Cup Winners' Cup ambapo iliupatia ubingwa huo nchini Sweden ikicheza dhidi ya Stuttgart ya nchini Ujerumani.
Sasa ni miaka 20 inatimia toka Chelsea kushinda taji hilo na ili kusheherekea miongo hiyo miwili ya ubingwa kumeandaliwa mchezo wa kirafiki ambao huu utawahusisha wachezaji na magwiji wa Chelsea watakaounda timu ya Chelsea Legends ili kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wakongwe na wachezaji wa zamani wa klabu ya Inter Milan ambao wenyewe wanajiita Inter Forever.
Mchezo huo wa kirafiki unachezwa usiku wa leo pale Darajani, Stamford Bridge huku nyota kadhaa wa kikosi kilichotwaa ubingwa huo wakiungana na baadhi ya nyota waliowai kupita klabuni Chelsea.
Dennis Wise, Gianfranco Zola, Roberto di Matteo, Gianluca Vialli na wengine wengi wataungana na nyota kama Eidur Gudjohnsen, Michael Ballack, Michael Essien, Willian Gallas na Hernan Crespo ambaye anaweza akacheza mchezo huo.
Mchezo huo ambao ni wa kirafiki ambao utachezwa kwa dakika 80 tu 40 kwa kipindi cha kwanza na 40 kipindi cha pili utakuwa umetengwa pia kwa kutoa heshima ya mwisho kwa gwiji na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Ray Wilkins ambaye alifariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu.
Chelsea: Gianfranco Zola, Dennis Wise, Gianluca Vialli, Graeme Le Saux, Tore Andre Flo, Roberto Di Matteo, Michael Ballack, Michael Essien, Eidur Gudjohnsen, Juliano Belletti, Marcel Desailly, Frank Leboeuf, Dan Petrescu.
Inter Milan: Francesco Toldo, Javier Zanetti, Jurgen Klinsmann, Marco Materazzi, Maicon, Giuseppe Bergomi, Giuseppe Baresi, Dejan Stankovic, Olivier Dacourt, Sebastien Frey, Christian Chivu.
Blog yako ya Darajani 1905 itakuletea ripoti na matokeo kamili kuhusu mchezo huu.
No comments:
Post a Comment