Ethan Ampadu kamili kurejea uwanjani - Darajani 1905

Ethan Ampadu kamili kurejea uwanjani

Share This

Ukifika klabuni Chelsea kwenye akademi ya klabu hiyo kuna nyota wanaotajwa kutazamwa kama nyota wa baadae kikosini hapo ambapo moja ya majina utakayotajiwa kuifanya Chelsea ijivunie ni pamoja na yule nyota raia wa Wales, Ethan Ampadu ambaye amekuwa na msimu mzuri tangu asajiliwe akitokea Exeter city mwaka 2017.

Nyota huyo aliichezea Chelsea mchezo wa kwanza dhidi ya Afc Bournemouth katika mashindano ya kombe la FA ambapo mwenyewe aliibuka kuwa nyota wa mchezo. Na baadae akitumika zaidi kwenye vikosi vya vijana wa Chelsea.

Nadhani ulimuona kwenye mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Liverpool wa hapo jana ambapo alikuwa kwenye orodha ya wachezaji wasiojumuishwa kwenye kikosi cha siku hiyo akiwa sambamba na nyota wenzake kama David Luiz na Danny Drinkwater ambapo sababu ya kutokujumuishwa ni kutokana na kuuguza majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa klabu bingwa kwa vijana ambapo Chelsea iliibamiza Real Madrid iliyokua nyumbani kwa mabao 2-5. Majeruhi hayo yakiripotiwa kumueka nje na hatoweza kurejea ndani ya msimu huu.

Na sasa nyota huyo anaonekana kuimarika zaidi mara baada ya kutuma ujumbe wa video kwenye mtandao wa Instagram akionekana akiwa kwenye bwawa maalum la maji na akijiendelea kujiweka sawa kwa kufanya mazoezi akiwa kwenye bwawa hilo maalum.

Hii inaweza kuwa ishara nzuri kwa nyota huyo kurejea rasmi uwanjani kwenye michezo ya kombe la mabingwa wa kimataifa maarufu kama International Champions Cup (ICC) ambayo itafanyika mara baada ya msimu kuisha na Chelsea huitumia michezo hiyo kama michezo ya kirafiki.

No comments:

Post a Comment