Nadhani kama sio kuamini kabisa kuwa jana ulipata maswali labda kwa kujiuliza mwenyewe au kuulizwa na wenzako juu ya kukosekana kwa mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata kwenye kikosi cha Chelsea ambapo hakukosekana kwenye orodha ya wachezaji 11 uwanjani tu, bali hata kwa wachezaji wa akiba jina lake halikuonekana kwenye mchezo wa jana kati ya Chelsea dhidi ya Liverpool ambapo Chelsea iliondoka na ushindi muhimu wa bao 1-0.
Lakini je ulipojiuliza ulipata majibu sahihi? au ndio ulikimbilia kudhania kama wengi wanavyodhania kama mchezaji aliyezoeleka kwenye kikosi alafu siku akakosekana ambapo dhahania ya wengi huwa ni mchezaji huyo kakosekana kutokana na majeruhi. Sasa hapa nakuletea majibu yenye uhakika juu ya mchezaji huyo kutojumuishwa kabisa kwenye kikosi cha Chelsea kwenye mchezo huo ambao Chelsea iliondoka na alama zote tatu.
Kocha Antonio Conte alifanya mkutano mfupi na waandishi wa habari hapo jana mara baada ya mchezo huo kuisha ambapo kati ya maswali aliyoulizwa ni pamoja na hili la kukosekana kwa mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la paundi milioni 60 katika dirisha kubwa la usajili lililopita ambapo alitua Darajani akitokea Real Madrid.
"Majeruhi ndio yaliyomfanya akakosekana ingawa sio ya kumweka nje kwa muda mrefu" alijibu kocha Antonio Conte alipoulizwa juu ya hatma ya nyota huyo.
Majeruhi ndio sababu iliyomfanya nyota huyo akakosekana kwenye mchezo huo ingawa yanategemewa ni ya muda mfupi na labda atakuwepo kwenye mchezo ujao dhidi ya Huddersfield.
*********
Bila kusahau zimesalia siku 12 kabla ya mashabiki wa Chelsea na wapenzi wote wa soka kukutana pale Hospitali ya serikali ya Temeke jijini Dar es Salaam ili kuifanya jamii yetu ifaidike kwa kupenda kwetu soka ambapo tutachangia damu kwa hiyari
#CharityForTheBlues
No comments:
Post a Comment