Alvaro Morata akubaliana na Juventus, abakiza kitu kimoja tu - Darajani 1905

Alvaro Morata akubaliana na Juventus, abakiza kitu kimoja tu

Share This

Alitua Chelsea kwa dau la paundi milioni 60 akitokea Real Madrid katika dirisha kubwa la usajili, na mpaka sasa ameshaichezea Chelsea michezo 39 na kuifungia magoli 15 ingawa nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza inaonekana kuwa hafifu tangu kuwasili kwa Olivier Giroud, aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Alvaro Morata anatajwa na moja ya magazeti ya nchini Italia kukamilisha makubaliano na klabu ya Juventus ambayo ipo tayari kumrejesha tena klabuni hapo ambapo aliwai kupitia kabla ya kurejea Real Madrid na sasa kutua Chelsea.

Gazeti hilo linaeleza kuwa klabu hiyo ya Juventus imeshafanya mazungumzo na mshambuliaji huyo raia wa Hispania na tayari washafikia makubaliano nyota huyo na kikubwa walichokibakiza ni kufanya mazungumzo na Chelsea ili biashara hiyo ikamilike.

Klabu hiyo inatajwa kukubaliana na nyota huyo kumpunguzia mshahara ili atue kwenye klabu hiyo na ilo linaelezwa kukamilika na nyota huyo aliyewai kuwa anatamani siku moja kurejea klabuni hapo amekubali akatwe ili ajiunge nayo.

No comments:

Post a Comment