Tarehe 25-Agosti-2018 itakuwa ni siku ya kulipiza kisasi kwa klabu ya Chelsea itakapokuwa ugenini kucheza mchezo wake wa tatu kwa msimu wa ligi kuu Uingereza 2018-2019.
Chelsea itakuwa ikicheza dhidi ya Newcastle United ambao walipata ushindi kwenye mchezo wa mwisho wa ligi kuu kwa msimu uliomalizika wakati Chelsea ikipoteza magoli 3-0 huku ikishindwa kukata tiketi ya kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao.
Matokeo na jinsi mchezo wa siku hiyo utategemea sana matokeo na jinsi klabu zitakavyojiandaa katika siku hiyo ingawa kiukweli Newcastle huwa ni mgumu pale anapokuwa nyumbani tena anapocheza dhidi ya Chelsea.
Katika michezo mitano ya mwisho ambayo Newcastle imecheza ikiwa nyumbani, Chelsea haijashinda mchezo hata mmoja huku ikiishia kuondoka na sare moja huku ikipoteza michezo minne wakati kiujumla katika michezo mitankmo ya mwisho wakati timu hizo zilipomenyana, Chelsea imeondoka na ushindi katika michezo mitatu na kupoteza mchezo mmoja huku mmoja huku ikitoa sare kwenye mchezo mmoja.
Tukirudi kwenye historia inasema katika michezo 163 ambayo klabu hizo zimekutana, Chelsea imeondoka na ushindi kwenye michezo 71 huku ikipoteza michezo 53 na ikitoa sare michezo 39.
Kupata habari zote kuhusu Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment