Jana ilikuwa siku ya mwisho ya michezo ya raundi ya 16 kuchezeka kwenye michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea huko nchini Urusi.
Katika siku hiyo Uingereza ndo ilikuwa timu ya mwisho kushuka uwanjani ikimenyana dhidi ya Colombia na kuishuhudia Uingereza ikikata tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali kwa ushindi wa penati au matuta na kumaanisha sasa timu hiyo itamenyana dhidi ya Sweden katika hatua ya robo fainali.
Uingereza yenye nyota wawili kutoka Chelsea imekamilisha timu nane zitakazocheza nusu fainali. Nyota hao ni Gary Cahill pamoja na Ruben Loftus-Cheek.
Lakini hii pia inamaanisha nyota nane kutoka Chelsea wamefanikiwa kufika hatua ya robo fainali. Nyota hao ni pamoja na N'Golo Kante pamoja na Olivier Giroud ambao wanaiongoza timu ya Ufaransa, Willian Borges da Silva atakayeiongoza Brazil, Gary Cahill na Ruben Loftus-Cheek watakaiongoza Uingereza pamoja na nyota watatu Eden Hazard, Thibaut Courtois pamoja na Michy Batshuayi kwenye timu ya Ubelgiji.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment