Winga na mlinzi wa kulia wa Chelsea, Davide Zappacosta anatajwa kukaribia kuondoka klabuni Chelsea huku wakala wake akihaha kumtafutia klabu nyengine itakayoweza kumpa nafasi ya kwanza tofauti na anavyotumika klabuni Chelsea akiwa anatumika kama mchezaji wa akiba.
Taarifa kutoka gazeti la michezo la kuaminika la huko nchini Italia linadai kwamba Chelsea inataka dau la euro milioni 30 kwa klabu ya Inter Milan ambao wapo tayari kumsajili muitaliano huyo.
Taarifa zinadai kwamba klabu hiyo ya Inter Milan inayotaka kujiweka sawa kwa ajili ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya imekataa kutoa dau hilo ambalo Chelsea inalitaka ili kumruhusu nyota huyo ajiunge na klabu hiyo ambayo nayo inapatikana nchini Italia.
Wakala wa nyota huyo anatajwa kufanya vikao vingi na viongozi wa Inter Milan na tayari makubaliano wameshahafikiana kilichobaki ni Chelsea kuamua kama itapokea pungufu ya hapo.
Kupata habari zote za Chelsea, tembelea kurasa zetu
Facebook➡Darajani 1905
Instagram➡darajani1905
No comments:
Post a Comment