Ngao ya Hisani; Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Manchester city - Darajani 1905

Ngao ya Hisani; Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Manchester city

Share This

Chelsea leo inashuka uwanjani kucheza mchezo wake wa kwanza wa kimashindano ambapo itakuwa uwanjani kucheza mchezo wake wa Ngao ya Hisani dhidi ya Manchester city.

Mchezo huo utakaochezwa mida ya saa 5:00 jioni (saa 17:00) kwa saa za Afrika Mashariki unaikutanisha Chelsea ikiwa kama bingwa wa Kombe la FA kwa msimu wa 2017-2018 ilipoibamiza Manchester united katika fainali kwa goli 1-0, goli lililofungwa na Eden Hazard wakati Manchester city akicheza mchezo huu akiwa kama bingwa wa ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2017-2018.

Kuhusu mchezo;
Mchezo huu unawakutanisha makocha wanaofanana kimbinu katika mtindo wa uchezaji ambapo wote (Maurizio Sarri kwa Chelsea na Pep Guardiola kwa Manchester city) wakitumia zaidi mtindo wa pasi fupi. Unalotakiwa kujua kuhusu mchezo huu ni kwamba utakuwa wa dakika 90 pekee na kama zikiisha bila timu kuondoka na ushindi basi zitapigwa penati au matuta ambayo yatapigwa kwa mtindo wa ABBA tofauti na mtindo wa kawaida uliozoeleka wa ABAB.

Mfumo wa ABBA hutumikakwa kwa mfano Chelsea ikiwa timu ya kwanza kupiga penati basi Manchester city watafata kupiga mara mbili mfululizo kisha tena Chelsea itapiga mara mbili mfululizo mpaka atakapopatikana mshindi. Mfumo huu ulitumika pia kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Chelsea dhidi ya Arsenal mwaka 2017.

Chelsea;
Nyota watano wa Chelsea ambao walishiriki Kombe la Dunia wataendelea kuukosa mchezo huu, Eden Hazard, Michy Batshuayi, Thibaut Courtois, N'Golo Kante na Olivier Giroud huku Cesc Fabregas akiukosa mchezo huu kutokana na majeraha aliyoyapata.

Mchezo huu ni wa muhimu zaidi kwa kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri ambapo kama akifanikiwa kuondoka na ushindi basi itakuwa ni mara ya kwanza kwake kushinda taji katika maisha yake ya soka.

Willian anaweza akatumika kwenye mchezo huu haswa kutokana na kurejea mazoezini tarehe mosi mwaka huu.

Manchester city
Safu ya ushambuliaji ya Manchester city inaweza kuongozwa na mshambuliaji wao mpya, Riyad Mahrez huku kwa upande wa Leroy Sane anaweza kutumika kwenye mchezo huu.

Mwamuzi;
Jonathan Moss ndiye mwamuzi katika mchezo huu huku jambo zuri likiwa katika michezo ambayo anakuwa mwamuzi basi Chelsea huwa na nafasi kubwa ya kupata ushindi. Michezo miwili ambayo alikuwa mwamuzi kwa msimu ulippita ilikuwa ni dhidi ya Swansea na Brighton & Hove Albion.

Muda; Saa 5:00 Jioni (Saa 17:00) kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment