Chelsea yashindwa kutamba, yakosa Ngao ya Hisani - Darajani 1905

Chelsea yashindwa kutamba, yakosa Ngao ya Hisani

Share This

Chelsea inapoteza mchezo wake wa Ngao ya Hisani ilipomenyana dhidi ya klabu ya Manchester city jioni ya leo. Mchezo ulioisha kwa magoli 2-0 yaliyofungwa na Kun Aguero.

Mchezo huo ulizikutanisha klabu mabingwa wa ligi kuu Uingereza na Kombe la FA ambapo Chelsea ndiye bingwa wa Kombe la FA huku Manchester city wakiwa ndio mabingwa wa ligi kuu.

Kipindi cha kwanza kilichezwa huku Chelsea akiruhusu goli la kwanza katika dakika ya 12 lakini ikifanikiwa kutawala mchezo na kusababisha kipindi cha kwanza kuisha Chelsea ikiwa nyuma kwa goli 1-0 huku goli la pili likifungwa na muargentina huyohuyo, Kun Aguero.

Mchezo unaofata
Chelsea vs Olympique Lyon
Siku; Tarehe 7-Agosti
Muda; Saa 22:05 (EAT)
Uwanja; Stamford Bridge-London, Uingereza

No comments:

Post a Comment