Karen Carney aibuka shujaa, Chelsea ikinusurika kipigo - Darajani 1905

Karen Carney aibuka shujaa, Chelsea ikinusurika kipigo

Share This

Mwanamama Karen Carney alikuwa shujaa kwa upande wa Chelsea FC Women hapo jana mara baada ya kuisaidia klabu yake kuondoka na matokeo ya suluhu katika mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Barcelona Ladies, mchezo uliochezwa huko nchini Hispania.

Karen Carney aliifungia Chelsea FC Women goli hilo akitumia kichwa dakika ya 90' ya mchezo na kufanya matokeo ya mchezo huo wa kirafiki kuisha kwa sare ya 1-1.

Huu ni mchezo wa pili wa kirafiki kwa Chelsea FC Women wakati mchezo wa kwanza uliochezwa huko nchini Ufaransa uliisha kwa klabu hiyo kupoteza kwa magoli 3-2 dhidi ya klabu ya wanawake ya Montrepillier.

Mchezo unaofata
Juventus Ladies vs Chelsea FC Women
Tarehe; 8-Agosti

No comments:

Post a Comment