Hazard kupewa mkataba mnono klabuni Chelsea - Darajani 1905

Hazard kupewa mkataba mnono klabuni Chelsea

Share This

Klabu ya Chelsea inaweza kumpa mkataba mpya nyota na winga wa klabu hiyo, Eden Hazard ambaye anaripoti klabuni Chelsea hii leo.

Chelsea inatajwa kuandaa mkataba mpya kwa winga huyo mwenye miaka 27 huku ikipanga kumpa mshahara unaotajwa kufikia paundi 300,000 kwa wiki huku mshahara wa sasa wa nyota huyo ukiwa unamalizika mwaka 2021.

Hazard ambaye aliongea na kocha Maurizio Sarri na kumuomba ruhusa ya kurejea klabuni siku ya jumatatu ya tarehe 6-Agosti badala ya kurejea siku ya jumapili ya tarehe 5-Agosti kama alivyopangiwa kutokana na likizo yake ya mapumziko kutokana na kushiriki Kombe la Dunia amekuwa akihusishwa mara kadhaa kuondoka klabuni hapo huku klabu ya Real Madrid ikihusishwa kwa karibu kumfukuzia.

No comments:

Post a Comment